Qwisah Atangaza Kuuaga Ukapera.

Mtangaza wa Clouds Media aliyejipatia umaarufu wake kupitia kipindi cha SHILAWADU akiwa na mtangazaji mwenzake Soud Brown, ametangaza rasmi kuuaga ukapera baada ya wikiend hii kumvisha pete mpenzi wake na kujianda kwa ajili ya ndoa hivi karibuni.

katika ukurasa wake wa instagram Qwisah aliandika “Siku ya Jumamosi ilikua ni siku kubwa Sana kwangu.. Nilifanya maamuzi makubwa Sana katika maisha maana nilijua itakua rahisi bt NO haikuwa Rahisi.. Nilienda mpaka kaburini kwa mama kwisa kuomba urahisi wa jambo hili na pia kuchukua baraka.. Nashukuru Mungu nilipo muomba MKE wangu matarajiwa Her hand in Marriage (Tuishi pamoja Milele) alinikubalia tena kwa furaha ya machozi juu (Hata mm nilikimbia chumbani kujifungia nilie kwanza, ?? si unajua kidume kulia hadharani tena..) Asante Sana kwa kila rafiki, ndugu na jamaa mlioweza kufika… Nyinyi ni familia yangu.. Mlikua wengi sintoweza kutaja mmoja mmoja.. Ila asanteni sana sana… Happy Birthday na Asante kwa kukubali kuishi milele na mm na watoto wetu.. Inshallah Jini mkata kamba yoyote asipite.. Damu itamwagika..” 

download latest music    

Hata hivyo  tangu alipoweka post iyo katika ukurasa wake wa instagram , mtandao huo umechafuka baada ya kila page ya udaku kuanza kumchambua mwanamke wake kila kona kama vile yeye na mtangazaji mwenzake Soudy wanavyokuwa wakifanya katika kipindi chake cha shilawadu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.