Rais wa Kenya azua utata kwa kunywa glasi moja ya bia kabla ya kuhutubia wananchi (Picha)

Rais Uhuru Kenyatta amezua utata baada ya kunywa glasi moja ya bia akiwa katika shuguli za kampeni jijini Kisumu siku ya Jumatano.

Uhuru alihudhuria ufunguzi wa kiwanda ya kutengeza pombe linalomilikiwa na kampuni ya East African Breweries Limited (EABL).

download latest music    

Rais huyo wa Kenya aliwekewa bia kiasi kwa glasi kuonja lakini yeye alisema ajaziwe glasi nzima ya pombe hio aina ya Senator Keg.

“Hiyo ni kidogo sana, ongeza ijae,” Uhuru aliambia mhudumu aliyekua akimwekea pombe.

Uhuru alimpea mhudumu huyo shilingi elfu mbili ya Kenya/ elfu Arobaini na tatu pesa ya Tanzania kwa kumhudumia.

Hatua ya rais Uhuru kunya pombe hadharani umezua utata kwani kuna wale wanasema rais hafai kunywa pombe hadharani.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere