Rama D afunguka kuhusu uhusiano wake na Lady Jaydee

Mwimbaji wa R&B Rama D ameweka kikomo kwa uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Lady Jaydee ni wapenzi.

Ukarimbu wa Rama D na Jaydee ndo ulichangia kuzuka kwa uvumi huo. Rama Dee na Lady Dee wamewahi kutoa wimbo pamoja ‘Kama Huwezi’ uliotoka mwaka 2013.

download latest music    
Rama D na Lady Jaydee

Staa huyu alikana madai kuwa yeye na Jaydee ni wapenzi katika mahojiano na Bongo 5. Alisema yeye anamchukua Jaydee kama ndugu wake.

“Lady Jaydee unafahamu ni mtu ambaye kwanza naweza kusema ni mtu ni rafiki wa kweli alafu rafiki wa kawaida. Mimi nashangaa tu, tumeshibana, tumeelewana  muda wote tunaulizana, sehemu tuliokosea tunaulizana…urafiki wa namna hio yani. Sasa hivi umefikia nadhani kama ndugu yangu. Kwasababu kwa muda wowote naweza kumpigia simu tukazungumza,” Rama D alieleza.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere