Rammy Galis Akiri Kuvutiwa na Irene Uwoya

Msanii wa filamu za Bongo movie Rammy Galis amefunguka na kukiri kuvutiwa kisanaana mrembo mkongwe kwenye tasnia Irene Uwoya.

Rammy amefunguka na kusema Irene ni mmoja tu kati ya wasanii wa kike ambao wanamvutia sana na sio kimuonekano tu Bali hata kikazi kumaanisha kazi zao za sanaa wanazofanya.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya katika kipindi cha The Playlist cha Times FM alipoenda kuzungumzia uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Hukumu itakayozinduliwa Disemba 15, 2018 City Mall Dar es salaam, Rammy Galis  amesema kuwa kila msanii anamvuto wake.

Kila mmoja ana mvuto wake ila nitake kusema anenivutia kwenye tasnia ya Filamu ni Rose Ndauka, Riyama Ally, Irene uwoya wapo wengi sana”.

Rammy alijizolea umaarufu Kupitia filamu zake kupenya hadi Nigeria lakini pia kwa mahusiano yake na Marehemu Agnes Masogange.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.