Rammy Galis Kumuingiza Mtoto Wa Masogange Kwenye Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie nchini Rammy Galis ametangaza kumuingiza kwenye filamu Mtoto wa Marehemu Agness Masogange ajulikanaye Kama Sania.

Rammy alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari siku chache zilizopita jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa filamu yake mpya aliyocheza na marehemu Agness Masogange, amesema kuwa amemshirikisha mtoto huyo kufatia kipaji kikubwa alichokiona ndani yake.

download latest music    

Nina mpango wa kumuingiza katika soko la filamu kwasababu mtoto wa Agness anakipaji kikubwa sana cha kuigiza na nitakua nae mwanzo hadi mwisho maana hata baba yake amekubaliana na suala hilo la mwanae kuingia kwenye sanaa”.

Lakini pia kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rammy pia ameweka wazi kuwa Mtoto wa Masogange ndio ameomba kuingia kwenye filamu Kama mama yake:

Rammy ameweka wazi kuwa  filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Desemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Citymall jijini Dar es Salaam itakwenda kwa jina la Hukumu ambayo aliamua kumshirikisha Masogange lengo likiwa ni kuhakikisha anamuhamishia katika upande wa uigizaji moja kwa moja.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.