Ray C Alinidhalilisha Sana Kwa Maneno Yake- Nandy

Mwanamuziki kutoka Jumba la sanaa la Vipaji THT, Nandy ameibuka na kudai kuwa alivunjika moyo kwa maneno ya udhalilishaji aliyoambiwa na msanii mwenzake Rehema Chalamila au maarufu kama Ray C.

Wiki chache zilizopita wasanii hawa wawili waliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni baada ya  Nandy kutumia/ kuimba nyimbo za Ray C katika tamasha la Fiesta ambapo hakulipwa kwenda kuimba. Ray C alimjia juu Nandy na kumwambia asitumie nyimbo zake kuingiza pesa kwani na yeye ni mwanamuziki hivyo anaweza kuimba nyimbo zake mwenyewe, jambo ambalo halikumpendeza Nandy ambaye alidai kuwa Ray C alikuwa na taarifa kuwa ataimba nyimbo zake kwani walikuwa wote THT kwenye mazoezi.

download latest music    

Nandy alipohojiwa na Dizzim Online, alisisitiza ya kuwa maneno yale aliyoyaongea mtandaoni yalimdhalilisha sana kama msanii

Sikuwahi kufikiria kama Ray C angeweza kupaniki kama alivyo paniki kwani hata mimi alinishangaza, baada ya yeye kuandika vile kwenye instagram, management yangu ilinipigia ili initulize kwa sababu kusema ukweli nilipaniki na nilijisikia vibaya sana pale watu walivyo nifata na kuanza kunitukana kwamba niimbe vinyimbo vyangu viwili na mambo mengine kitu kilichonidhalilisha sana pia kwa sababu nilivyoimba ile nyimbo sikuimba kwa ubaya ilikuwa ni kwa nia nzuri tu ya kuburudisha mashabiki zangu”.

Tangu ishu hii itokee Nandy amekuwa mtu wa kuizungumzia sana akionyesha kuwa hakufurahishwa hata kidogo tofauti na Ray C ambaye hajawahi kuongelea suala hili hata mara moja

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.