Ray C Awapa Moyo Wasanii Wakongwe

Mwanadada aliwahi kuvuma sana katika tasnia ya bongo fleva mwenye kiuno chake bila mfupa amefunguka na kusema kuwa kuna jini limekuwa likiwasumbua sana wasanii wa muziki hasa wakongwe  na kushindwa kuendelea na muziki wao.Ray C aliyasema hayo baada ya shoo wa Lady Jay Dee kubadlishiwa ukumbi  siku anazindua project yake ya anaweza ambayo ilifanyika wikiendi iliyopiata jijin Dar Es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Ray c aliongea hayo baada ya kubadilika kwa ukumbi alitakiwa kufanyia shoo lady jay dee na kisha kuhoji yuko wapi mtu kama Marlow, Mandojo na Domo Kaya, juma nature , anasema kuwa anahisi kuna jini anawavuruga wasanii wakongwe.

download latest music    

Kuna nini bongo fleva, wasanii wapya ni wengi, ooh yes nalijua hilo lakini ukweli ni kwamba nchi yote hapa afrika mashariki nikienda nasikia tu nyimbo za zamani,mimi mwenyewe pamoja na mahanjumat ya pepo la ahera lakini bado sauti ipo nje.nasikia kuna jini mmoja ambae amekuwa akiwafanya wasanii wajione kuwa ndio basi tena.point yake ni moja kuwa anauwezo wa kukujenga na kukumaliza mara moja , jini huyo ni promota.

Ray c anaendelea kuwapa moyo wasanii kwa kuwaambia kuwa hata ingekuwaje lakini wanapaswa kujua kuwa kipaji ndio kila kitu na wala hawana haja ya kuhofia kuhusu watu wengien kama mapromota.

wasanii mna kazi kubwa ya kujiamini kwanza kabla ya kumuamini mtu mwingine,mkishajua aliyewapa viapaji basi mtasimama tena.maana mashabiki wenu bado wapo,kinachohitajika ni kipaji na wala sio promota.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.