Ray Kigosi Awapa Somo Viongozi wa Wasanii Walioteuliwa na BASATA.

Msanii wa filamu nchini, Vincent Kigosi (Ray Kigosi) amewataka wajumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mwana FA pamoja na single Mtambalike ‘Richie’ ambao wameteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, kutojisahau kwa nafasi walizopewa.

Akiwa kwenye interview Ray amesema “nimefurahi kwa uteuzi huu lakini ningefurahi zaidi kama pale BASATA na Bodi ya filamu wangekaa watu ambao wanajua kila kitu kuhusu sanaa, nimshukuru sana Waziri kwa kuwateua Mwana FA na Richie, ila niwaambie tu wasijisahau watusemee sisi na sio wajisemee wao ili tuweze kupiga atua kisanaa

download latest music    

Wasanii hawa wameteuliwa wakiwa kama wawakilishi wa wasanii wengine kaatika bodi ya BASATA ili kufanikisha utatuaji wa matatizo ya wasanii.

Ray kwasasa amekuwa kimya sana kwenye gemu ya filamu lakini amewaahidi mashabiki zake kuwa anawaletea kitu kipya hivi karibuni

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.