Ray Kigosi:Niko Tayari Kumuita Dogo Janja Shemeji kwa Uwoya

Msanii Vicent Kigosi maarufu kama Ray, amefunguka na kusema kuwa yeye hana wivu wowote na msanii mwenzie Irene Uwoya ambae hivi karibuni alifunga ndoa na msanii wa bongo fleva Dogo Janja.Ray ambae ndie alikuwa mtu wa kwanza kumfungulia Irene Uwoya milango ya sanaaa katika tasnia hiyo anasema kuwa hana wivu kabisa na mwanadada huyo kuolewa kwa sababu kati yake na Dogo Janja yeye ndie alikuwa wa kwanza kumuona hivyo kama angetaka kuwa nae katika mahusiano angekuwa ameshamchukua siki yingi kabla yake .

Mimi siwezi kuwa na wivu  nilianza kumuona irene uwoya kabka hata ya Dogo Janja, Dogo Janja ni mdogo wangu lakini pia naheshimu maamuzi yake ya kumuoa Irene Uwoya.Mimi yule ni dada yangu ambae tumetoka nae mbali sana kwenye sanaaa, na mimi ndie nilimu-introduce Irene  kwenye sanaa nikiwa na marehemu Kanumba.Kama ningekuwa nimemuona na ningekuwa nimemtamnai basi ningekuwa nae  lakini niliamua kufanya nae kazi tu, wengine wamemuona na wamemchukua ilo ni jambo zuri hata Mungu pia anafurahi. -Alifunguka Vicent Kigosi

Lakini pia Ray ameongezea kuwa kwake yeye yupo tayari kumuita Dogo janja shemeji kwa sababu alishachukua jukumu la kumuoa dada yake Irene Uwoya hivyo hana kipangamizi chochote na hana sababu ya kukataa kwa sababu ndoa ni jambo la kheri.

download latest music    

Mapenzi ni kipenda roho na kipenda roho hula nyama mbichi,kama wamependana wenyewe inatosha .mimi niko tayari kumuita shemeji kwa sbabu tayari kamuoa dada yangu -Aliongezea Ray Kigosi

Dogo Janja na Irene Uwoya waliingia katika headlines za vyombo vya habari baada ya kufunga Oktoba 28 mwaka huu  , ambapo watu wengi wameshikwa na butwaa kwa ndoa iyo kutokana na umri wa wawili hao kuwa umetofautiana sana ,lakini pia wawili hao walikuwa wakikanusha kabisa kipindi cha nyuma kuhusu mahusiano yao.Hata hivyo wenyewe wamethibitisha kupendana hata kama kuna utofauti wowote uliopo.

Ray ambae pia yupo katika mahusiano na msanii mwenzie wa filamu Chuchu Hans wamefanikwa kupata mtoto mmoja wa kiume.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.