Rayvanny aisuta Basata kwa kukosa kuenda kumpokea katika uwanja wa ndege

Rayvanny alipewa mapokezi ya kirais alipowasili Tanzania kutoka Marekani. Staa huyu wa Wasafi alishinda tuza la BET na kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hilo.

Diamond, Harmonize, Babu Tale na mamia ya mashabiki walijitokeza kwa wingi kumlaki Rayvanny katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere.

download latest music    

Rayvanny ata hivyo ameisuta Basata kwa kukosa kuenda kumlaki katika uwanja wa ndege, alisema bodi hio ya sanaa nchini haikuonyesha picha nzuri na hatua yao.

“Kwa mafano, mimi nilivyochaguliwa kama BASATA walikuwa wameona. Wao ni wazazi walikuwa na chochote cha kusema lakini wakisema kwamba wanasubiri niende mimi mwenyewe au tunasubiri watuambie au hatuwezi kwenda kwa sababu hatujaambiwa. Wale ni wakubwa kwetu ni wazazi wetu tunategemea kwamba wanakuza sanaa yetu na sisi tunawaangalia wao walitakiwa kuwa kipaumbele sisi kutusaidia,” Rayvanny alisema.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza akiongea na Clouds FM alitetea bodi hilo kwa kusema kuwa Basata haikupata ratiba ya Rayvanny.

“Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee,” Godfrey Mngereza alisema.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere