Rayvanny akamilisha kazi yake mpya na Jason Derulo

Mkali wa Wasafi Records Rayvanny hatimaye aliweza kukutana na Jason Derulo marekani ambapo wawili hao waliweza kukamilisha kazi yao mpya itakoyoachiliwa hivi karibuni.

Rayvanny alijumuika na Jason Derulo siku kadhaa baada ya kushinda Tuzo lake la kwanza la BET. Kupitia mtandao wake wa Instagram Rayvanny aliweka picha yake na Jason Derulo huku wakionekana wakiwa kwenye studio session.

download latest music    

Aliandika kusema,

“God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui… Studio kulikua na Watoto wakaaaaaliiiii lakini kawacha waondoke sababu walichoka kukaa studio yeye kabaki na sisi tu. Naamini kilichofanyika Mtakipenda. Thanks boss @afrikidd @babutale.”

Tazama picha hiyo Hapa;

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua