Rayvanny aweka picha akiwa na mwanae, huu ndio ujumbe aliomwandikia

Image: Rayvanny na mchumba wake

Msanii kutoka label ya Wasafi records Rayvanny sasa hivi ni baba ya mtoto mmoja wa kiume, Jayden. Jayden ambaye alizaliwa na Fahyma mwezi wa Aprili mwaka huu amewaletea wazazi wake furaha na Rayvanny hawezi ficha mapenzi aliyonayo kwa mtoto huyu.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Rayvanny aliweka picha akiwa na mtoto wake huku akiandika kusema,

download latest music    

Mimi na pacha wangu @jaydanvanny

Japo bado Fahyma na Rayvanny hawaonyesha uso wa Jaydan wengi wana imani kuwa mtoto huyu anafanana na babake kwani rangi yao pia inafanan. Lakini mashabiki wao wanangojea Arobaini ya Jaden kuona kama watamuonyesha mtoto huyu.

Hata hivyo, tazama picha hiyo hapa:

Rayvanny akiwa na mwanae

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua