Rayvanny na Fahyma Hawajaachana Bali Walipishana Kauli- Babu Tale

Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka kuhusu sakata lilitokea kati ya msanii kutoka WCB Rayvanny na Mama watoto wake Fahyma.

Siku chache zilizopita Rayvanny na mpenzi wake Fahyma walitawala headlines na kutrend kwenye mitandao ya kijamii baada ya wawili hao kurushiana maneno na kupelejea watu kudhani kuwa labda wawili hao wameachana.

download latest music    

Tetesi za michepuko kuhusishwa kwenye ugomvi huo zilitawala hasa baada ya Rayvanny kuanza kurusha picha za wasichana wengine lakini kilicho washangaza watu wengi ni kitendo cha wawili hao kugombana na kuamua kuachana kwenye Instagram.

Babu Tale ambaye ni Meneja wao alifunguka na kudai sio kweli kuwa wawili hao wameachana ila tu kilichotokea ni walipishana kauli na kutoelewana kidogo.

Kwenye interview na Soudy Brown kupitia kipindi cha XXl cha Clouds, Babu Tale alifunguka yafuatayo:

Kusema ukweli hata mimi naona mnachoona nyie mitandaoni nikimuuliza vipi kunani anacheka tu namwambia hapa kuweni makini mmezaa msilete ujana kwenye maisha ya ndoa hata kama mkiwa hamjaoana lakini mtoto wenu bado mdogo kwaiyo manya mzaha au mnapogombana kuweni making lakini mwenyewe akaniambia hawajagombana walipishana kauli tu Mimi nikamshauri awe makini tu lakini ndio mapenzi ya mastaa hayo ila baadae nawaona wanaongea kwenye video call ila mimi sijataka kuwaaingilia maana nisije kuwa naletewa kesi kila siku bure”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.