Rayvanny:Maisha Ndani ya WCB Sio Mabaya

Moja ya wasanii wanaotoka WCB, Raymond maarufu kama Rayvanny amefunguka na kuzunguzmia maisha mazuri ndani ya WCB na mishahara mikubwa wanayolipwa inayowafanya wapende kufanya kazi kwa kujituma na kuzipenda kazi zao kwa ujumla.

Rayvannya anasema kuwa kwa upande wa wasnii kutoka WCB na wafanyakazi wote wa lebo hiyo wamekuwa wakifanya kazi vizuri na kujituma sana kwa sababu boss wao amekuwa akiwalipa vizuri sana na maisha yao yamekuwa yakiwanyiikea kila siku kiasi kwamba kila msanii au mfanya kazi wa wcb amekuwa na uwezo wa kulinga na kujigamba kuhusu maisha yake na pesa zake ingawa watu wengi wamekuwa wakisema kuwa kujionyesha na fedha hizo ni sawa na kuwalingishia wengine.

download latest music    

Akiongea na Global Pulblisher , Rayvanny amesema kuwa boss wao huyo (Diamonnd) amekuwa akiwalipa marupuruku na posho za shoo vizuri sana na hicho ni kitu  kikubwa wanachojivunia sana wanapokuwa wcb.

Kutokana na maisha mazuri ndani ya wcb  ndio maana utaona kuwa siku hizi anaweza kutokea msanii yoyote kutoka ndani ya wcb na akaweza kusema na kutaja kiwango cha pesa wanacholipwa na boss wetu  na maisha mazuri tunayopatiwa, jambo ambalo watu wengi wamekuwa wakiona kuwa tunajigamba lakini ukweli ndo huo kuwa maisha ndani ya wcb sio mabaya.

Hata hivyo rayvanny amekiri kuwa swala la harmonize kusema kuwa sasa hivi ana hela sana ni kweli huo unakuwa ni kama ushuhuda wake kwa kazi nzuri anayoifanya inayomfanya alipwe vizuri hivyo ni kweli kuwa wana hela sana siku hizi.

swala la Harmonize kuwa anasema sasa hivi ana hela huo ni kama ushuhuda kwake,kwa sababu kla mtu anakuwa na njia yake ya kutoa ushuhuda, juu ya jambo analotendewa  au alilokuwa akitendewa katika maisha yake  nyuma au anayoendelea kutendewa sasa.

Hata hivyo rayvannya anasema kuwa boss wao huyo amekuwa ni mtu wa kuwaomba na kuwahimiza kufanya kazi vizuri sana na kwa kujituma ili waweze kuweka ela nyingi katika akaunti ya lebo yao huku yeye bosi akiwa akatwi hata senti kumi.

Wasani hao kutoka lebo kubwa nchini ya WCB, chini ya boss wao Diamond Platinumz wamekuwa ni wasanii wanaofanya vizuri sana kwa sababu ya kujituma kwao  na pamoja na kwamba wasanii hao hawana muda mrefu sanatangu kutambulika katika game la muziki lakini wamekuwa wakifanya vizuri na kufanikiwa kupenyeza muziki wao mpka nje ya Tanzania.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.