Rc Makonda aanda Mpango wa Kumsaidia Chid Benz

Baada ya ukimya mrefu kwenye game ya Bongofleva, Rapa Chid Benz ‘Chuma’ ameeleza kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ameamua kumsapoti katika kazi zake kwa mwaka 2019.

Akifanya mahojiano na moja ya Tv kubwa nchini Tanzania Benz amesema kuwa “Mh Makonda mi namuita Paul ameamua kunisaidia mdogo wake, kaniambia Chidi hakuna kuona aibu ongea na watu wako, sema waambie watuchangie mimi nguvu yangu itakuwa ndogo bado inahitajika nguvu ya watu wengine”
Kuhusu mipango mingine waliyoizungumza na Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam, Chid amesema kwa sasa hatoizungumzia sana bali anamuacha kiongozi huyo afanye kwanza kwa kuwa yeye ndiye ameamua kuiweka mipango hiyo.

download latest music    

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.