RC Makonda Aanika Picha Za Mtoto Wake Hadharani

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameweka wazi Picha za  mtoto wake Keagan aliyezaliwa Miezi michache iliyopita.

Siku ya jana RC Makonda na Mke wake walikuwa wanafikisha miaka saba ya ndoa katika kusheherekea hilo Makonda amemuweka mtoto wake hadharani.

download latest music    
.
.

Kipitia ukurasa wake wa Instagram, RC Makonda ameandika ujumbe huu:

“Ni miaka saba ambayo MUNGU ametupa Baraka na zawadi ya kipekee, pamoja na uhai MUNGU aliotupatia lakini kwa wanandoa MTOTO ni moja ya zawadi kubwa ambayo wanandoa huitegemea, huiomba na kumlilia MUNGU usiku na mchana waweze kuipata, leo namshukuru MUNGU ninayo furaha kubwa kusherehekea miaka saba ya ndoa yangu nikiwa na mtoto wa kiume anaejulikana kwa jina la KEAGAN.

Namshukuru MUNGU kwasababu haikuwa rahisi, na najua kuna wengine ambao wamekata tamaa ndani ya mwaka mmoja, miaka miwili au mitatu, na wengine hata ndoa zao kuvunjika kwasababu ya kutokupata mtoto, lakini jawabu la MUNGU hutoka kwa wakati wake.

Naendelea kumshukuru sana MUNGU kwa kunipa mke mwema aliepita nami katika mabonde na milima, hata pale Dunia iliponiacha peke yangu, MARIA WANGU hakuthubutu hata kwa sura kuonesha hayuko pamoja na mimi, naendelea kumshukuru zaidi hata niliporudi kazini nikiwa naweweseka sijui hili wala lile alionesha tabasamu na kuniambia MUNGU YUPO.

Hata hili tutavuka mume wangu’ alinifuta machozi usiku wa manane pale nilipopaza sauti na kumlilia MUNGU nae akiwa pembeni akisema nitasimama na wewe tutaomba pamoja, pale ninapoamka asubuhi na kukuta magazeti yamechafuka na kuandika kila aina ya habari bado mke wangu alisema BADO NAMUAMINI MUNGU HATA HILI ATAKUVUSHA.

Pale nilipokaa na kuona mitandao ya kijamii ikinisema kwa kila namna na wengine kwenda mbali zaidi na kutoa kila aina ya matusi, lakini bado mke wangu hakuweza kukata tamaa, aliendelea kuniamini, kuniombea na kunishika mkono, amefanyika kuwa jua pale nilipohitaji muangaza, amefanyika kuwa maji pale nilipohitaji, alifanyika kuwa kila unachokijua kuhakikisha kwamba sikati tamaa.

Na kwa hilo sina zaidi ya shukurani za kipekee kwake, nafahamu hakika umri wangu wa ndoa sio mrefu kuliko wewe na wengine ambao wako katika ndoa miaka kumi, ishirini au thelathini, lakini kwa yake niliyoyapitia inatosha kusema ASANTE MUNGU KWA KUNIPA MKE MWEMA. Kipenzi changu Maria, wewe ni Jua langu, mwezi wangu , amani yangu, pepo yangu, kipenzi changu“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.