RC Makonda Ampa Milioni 5 Mama Yake na Godzilla

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amesema atampa pesa kiasi cha Tsh milioni tano, mama mzazi wa aliyekuwa Rapa wa Bongo, marehemu Golden Jacob Mbunda ‘Godzilla’ ili zimsaidie katika kuwatunza watoto wa marehemu.

Godzilla alifariki ghafla Wiki iliyopita Baada ya kuugua ambapo ameacha familia inayomtegemea ikiwemo Mtoto Wake na Mama yake mzazi.

download latest music    

Makonda alisema hayo  Jumamosi, Februari 16, 2019 katika Uwanja wa Salasala wakati akitoa salam za pole kwa familia, ndugu na wasanii kwa kuondokea na msanii huyo aliyeaga dunia usiku wa kuamkia Februari 13, mwaka huu.

Ndugu yetu alikuwa na mipango wa kumsaidia mama yake kiuchumi, akawa amempa milioni nne lakini akawa na malengo ya kumpa milioni tano  ili aweze kuanzisha famasi kama sehemu ya kujitengemea kiuchumi.

Nitampa mama mzazi wa marehemu Godzilla kiasi cha shilingi milioni tano, nitampa Fid Q azilete kwa Mama Jumatano ili zimsaidie kuwatunza wajukuu na kufanya kile alichopanga baada ya kutumia pesa nyingi katika atibabu ya Godzilla”.

Mwili wa Godzila umezikwa jijini Dar Es Salaam katika makaburi ya Kinondoni. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.