RC Paul Makonda Amwagia Misifa Lukuki Wema Sepetu

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameshindwa kujizuia na kumwagia Misifa Lukuki msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kujishindia tuzo ya muigizaji bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Tangu Wema ashinde tuzo hiyo siku ya jumapili Kumekuwa na maneno maneno mengi hasa kutoka kwa wasanii wenzake wa Bongo movie ambao wameona kuwa hajastahili kushinda tuzo hiyo.

download latest music    

Paul Makonda amemwagia sifa hizo Lukuki Wema na kuwajia juu wale wote wanaoziponda tuzo hizo zilizoandaliwa na Azamu Tv na kudai watu hao hawana hata uwezo wa kuandaa tuzo za kuku.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Paul Makonda alimwagia Wema sifa hizi:

Naomba picha uliopokea Tunzo kwa sababu nimesikia maneno maneno kwa watu wasioweza hata kuandaa tuzo za kuku. Hongera Azamu Tv mmefanya kuliko hata matatajio ya watu. Endeleeni kufanya vyema ili mwakani mpokee tuzo tena na wale wenye kukosa endeleeni kukosa ili mwakani mkose tena. Huu ndio Utamaduni unaofanya wenye kufanikiwa wachukiwe na wenye kuchukia kujifariji kwa maneno bila kuweka bidii katika kazi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.