Reality TV star wa Kenya Mishi Dorah adai kuwa Rayvanny alitaka kumpa mimba

Kilichotokea kati ya Mishi Dorah na Rayvanny hakiwezi julikana kwa kiukweli kwani wawili hao walikutana wakati ambapo hakuna yeyote alijua kuwa wana ‘mahusiano.’

Mishi Dorah

Hata hivyo, Rayvanny amekuwa akimkana mwanamke huyu kwa kusema kuwa anataka kumuharibia nyumba na jina lake. Lakini baada ya Ghafla kumhoji mwigizaji huyo wa Nairobi Diaries, Mishi Dorah alisema kuwa ni kweli aliweza kupatana na Rayvanny kimapenzi.

download latest music    

Mishi Dorah aliendelea kwa kusema kuwa hajapata hedhi zake kwa mwezi mmoja kuonyesha kuwa kunauwezekano wa mwanamke huyu kuwa na mimba ya Rayvanny kutokana na alivyosema. Kulingana na Mishi, Rayvanny alikuwa anataka sana wawili hao wapate mtoto wao wa kwanza kitu ambacho alihisi hawezi kuharikisha kwani hakutaka kuiharibu figure yake.

Lakini swali bado ni…Kati ya mwanamke huyu na Rayvanny nani anasema ukweli? Ebu itazame interview yake hapa.

https://youtu.be/wN6ppPh-TEI

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua