Rich Mavoko na Lulu Diva Waanika Penzi lao Hadharani

Msanii wa Bongo fleva kutoka label maarufu kabisa Tanzania Wasafi Classic Group (WCB), Rich Mavoko amejikuta anashindwa kujizuia na kuanika penzi lake na msanii mwenzake wa Bongo fleva Lulu diva.

Rich Mavoko na Lulu Diva wamekataa mara kwa mara habari za wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi ingawa habari hizo zimekuwa hazichezi mbali nao kila uchao.

download latest music    

Habari za wawili hawa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zilianza kusikika tangu mwaka jana ingawa kila mmoja wao amekuwa akikwepa tuhuma hizo na kudai hawana ukaribu wowote bali ni watu walio katika tasnia nyingine.

Siku ya Jumapili kampuni nzima ya WCB walikuwa wanamtambulisha rasmi msanii wao mpya ambaye wamemsaini ambaye ni Maromboso au Mbosso katika hafla hiyo matukio mbali mbali yalikuwa yanaendelea moja ya tukio lililowavutia watu wengi ni ukaribu uliokuwepo baina ya Lulu diva na Mavoko.

Wawili hao walionekana wakiwa wamekaa karibu sana (zero distance) huku mara chache chache walikuwa wakiwekeana mikono kama ishara ya kukumbatiana na kwa wakati huo wakiwa ndani ya maongezi mazito.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kuwa Lulu diva kaachwa na sponsor wake anaye muweka mjini kisa ni mahusiano yake na Rich Mavoko lakini kama kawaida yao wawili hao walikataa tetesi hizo na Lulu diva kudai yeye ana mpenzi wake na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Hizi baadhi ya picha walizopigwa Rich Mavoko na Lulu diva siku ya tukio:

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.