Ringtone Amchana Zari Baada Ya Tetesi Za Kurudiana na Diamond

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka 254 Kenya Ringtone Apoko amemjia juu Zari baada ya kuanza kusikika kwa tetesi kuwa amerudiana na Diamond.

Ringtone alishika headlines mwezi uliopita baada ya kukiri kumzimia Zari na kudai yupo tayari kumuoa na hata kumnunulia gari aina ya Range Rover mpya ambayo Zari aliikataa.

download latest music    

Lakini sasa Ringtone amerudi kumhoji Zari kuhusu Tetesi za yeye kurudiana man Diamond Ikiwa alishatangaza kuwa wameachana na hawezi kurudi kwake Tena.

Siku ya jana kuna Tetesi zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zari na Baby dady wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz wamerudiana baada ya kutengana kwa takribani Miezi minne.

Ringtone amemtolea povu Zari kwa uamuzi wake wa kuamua kupasha kiporo na Diamond ambapo amempa maneno haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Mpendwa Zari huwezi ukaendelea kusoma kurasa za kitabu kile kile kila siku ilihali unajua kitakavyoishia, ulioandoka Misri ukaenda Kanani itasikitisha kama utarudi tena.

Nini kitatokea kwa wasichana kibao uliowaambia sasa unamjenga Zari? Ushauri wangu ni kuwa hivi sasa mtafute Mungu kwa kufunga na maombi ili Mwenyezi Mungu akupe mwelekeo.

Lakini hivi sasa hatuna wasiwasi maana wote tunajua huwezi kurudiana na Diamond”.

 

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.