Roma: BASATA Nipunguzieni Adhabu Mtaniua Njaa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap Roma Mkatoliki amefunguka na kuiangukia kwa mahojiano BASATA huku akiomba apunguziwe adhabu.

Mwezi uliopita Roma pamoja na wasanii wenzake wa Bongo fleva walifungiwa nyimbo zao na BASATA kwa kudai maudhui yake hayana maadili ya Kitanzania, lakini Roma alitangazwa kufungiwa kabisa kufanya sanaa kwa muda wa miezi Sita.

download latest music    

BASATA ikiwemo wazi kuwa imemfungia Roma kutokana na wimbo wake wa ‘kibamia’ ambao walimwambia mara kadhaa aubadilishe lakini aligoma na kila walivyomuita alikataa kutokea.

Siku ya jana Roma na mtoto wake Ivan walifanya Interview na XXL ya Clouds Fm na aliomba BASATA impunguzie adhabu yake kwani hali yake ya kiuchumi sio njema kabisa:

Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee

Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja”.

Lakini pia kilichokamata hisia za watu wengi ni pale mtoto wa Roma, Ivan alipoulizwa kwa nini hakwenda shule siku ile ndipo alipojibu “Sijakwenda shule leo Baba hana hela”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.