Rose Ndauka Adaiwa Kutapeli Pesa

Muigizaji wa Bongo movie Rose Ndauka amepatwa na skendo nzito ya utapeli ambapo amedaiwa kumtapeli mfanyakazi wake kiasi cha shilingi laki na nusu.

Kipindi cha Shilawadu cha Clouds Fm wanaripoti kuwa mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Stumai amemtuhumu Rose kwa kumdhulumu kiasi hicho cha pesa baada ya kumpa huduma.

download latest music    

Kwenye Interview na kituo hicho mwanadada huyo anafunguka kuwa aliajiriwa Kwenye moja ya saluni za Rose Ndauka lakini baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu alikataa kumlipa na kudai hajaona faida hivyo avumilie atakuja kumsaidia kuwa supastaa.

Baada ya povu hilo Soudy Brown alimtafuta Ndauka ambaye alimwaga povu zito kwani hakufurahishwa na taarifa na kumtolea maneno haya:

Kama kesi inahusu wafanyakazi nenda Kwenye wizara ya Ajira na wafanyakazi sio Shilawadu, Soudy wewe ni mshkaji wangu Sitaki kupizana Kelele na wewe nina stress nyingine za maisha za Familia lakini stress nyingine za kujiunga za kipumbavu kama hizo sitaki kuziongelea kabisa”.

Mwishowe Rose amemtaka dada huyo aende mahakamani akashtaki au anaweza akaenda alipokuwa anafanya kazi Mwanzoni.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.