Rose Ndauka Amtaka Mc Pilipili Afunguke Mahusiano Yao

Mwandada Rose Ndauka amefunguka na kumtaka mc pilipili kufunguka mbele ya hadhara kuweka wazi mahusiano waliyowahi kuwa nayo na hata walionayo sasa kwa sababu kumekuwa na habari mtaani kuwa moja ya watru walioumizwa sana na kitendo alichokifanya Mc pilipili wikiend hii cha kumvisha pete mchumba wake kimemuumiza sana.

Rose anasema kuwa yeye na mc pilipili wamekuwa marafiki na wafanyakazi kwa muda mrefu sana lakini hakuna mahusiano ya mapeniz kati yao kamavile watu wanavyosema katika mitandao ya kijamii,

download latest music    

Akitoa salamu za pongezi, rose alisema kuwa pamoja na kwamba anatoa salamu zake za pongezi lakini ukweli inabidi ujulikane kwa watu na kwamba hakuna mahusiano ya kimapenzi baina yao.

Rose ndauka aliandika “Hongera sana mshikaji wangu kwa kupata mwenza lakini naomba kama itakuwa vizuri siku moja kuweka ukweli maana msema kweli ni mpenzi wa mungu…jamani ni hivi haijawahi kutokea mimi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mc pilipili……. ”

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.