Rose Ndauka Kuangalia Fursa Nyingine Mbali na Filamu

Muigizaji wa filamu za Bongo Movie Rose Ndauka amefunguka na Kuvunja ukimya baada ya kutosikika na kutoonekana akifanya kazi yoyote ya kisanaa kwa muda mrefu.

Rose amefunguka na kuweka wazi kuwa ameamua kuweka sanaa kando kwa sasa na kuelekeza nguvu zake Kwenye shughuli nyingine kutokana na majukumu yake kuongezeka.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Gazeti la Amani, Rose alisema kuwa mtoto wake sasa hivi anakua na anahitaji mahitaji muhimu kama elimu bora na vitu vingine vingi hivyo lazima aangalie upande mwingine wa kufanya kitu mbali na filamu ila maisha yazidi kusonga mbele.

Unajua Naveen anakua, sasa nikisema nikalie kazi moja ni ngumu sana, sasa hivi nimefungua House Beuty kwa ajili ya kupamba wanawake na masuala mazima ya urembo, kazi hii inaniongezea kipato na huku nikiendelea mdogomdogo na filamu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.