Rose Ndauka :-Mc pilipili Alikuwa mtu wa Masihara

Mwanadada msanii wa bongo movies, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na mchekeshaji Mc pilipili kama ambavyo imekuwa ikizushwa katika vyombo vya habari, Rose anasema kuwa mara zote alikuwa akichukulia kama swala la utani.

Mc Pilipili baada ya kumvisha pete mchumba wake mpya, watu walisema kuwa Rose ndauka anakuwa moja kati ya wasichana wanaumia sana na swala hilo kwa sababu aliwahi kutoka nae kimapenzi Mc Pilipili.

download latest music    

Mc pilipili nilikuwa nafaya nae kazi Times Fm na alikuwa kila mara ni mtu wa masihara tu  sijawahi kumcukulia kuwa serious kabisa, kwaio sijawahi kuhisi kitu kama ananipenda wala kama alikuwa akinitaka kimapenzi.

Akiongea kuhusu swala la kwenda kutambulishwa kwao Dodoma, Rose anasema kuwa ndio aliwahi kwenda Dodoma lakini ilikuwa ni kikazi tu na wala sio vingine kwa sababu waliweza kwenda Dodoma na kufanya kazi na kila mtu alifikia katika hotle yao na walikutana tu ukumbini.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.