ROSTAM Waipania Fiesta 2018

Wasanii wanaounda kundi la rostam, Roma na Stamina wameonyesha manjonjonyao na jinsi walivyojipana katika kufunika tena fiesta ya mwaka 2018 kama walivyofanya hapo mwaka uliopita kwa mashabiki zao kwa show zao za kibabe.

Wasanii hao wameongea hivyo walipokuwa wakitambuisha wimbo wao mpya katika vituo vya clouds media na kusema kuwa mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu ukimya wao walikuwa wakijipanga jinsi ya kuendelea kuwaburudisha  na wala kundi halijavunjika.

download latest music    

Hatukuwa kimya tu bila kuwa na sababu, tulikaa kimya ili kuja na kitu tofauti na kweli tumekuja na kitu tifauti.watu wasiubiri tu waone jinsi tutakavyo wapagawisha katika fiesta ni zaidi ya mwaka jana.

Kundi hili limeanza kufanya kazi zake mwaka uliopita lakini walikumbwa na misukosuko ya BASATA hapo katikati baada ya kutoa wimbo usiokuwa na maadili kwa jamii, hata hivyo kundi hili linafanya vizuri na wameanza kufanya kazi na wasanii wa nje.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.