Sabby Angel Adai Anabebea Mimba Mastaa Kwa Mil.20

Msanii wa filamu za Bongo Movie Sabrina Omary maarufu kama Sabby Angel ameibuka na kudai kuwa Yupo Tayari kubebea mimba mastaa ambao hawana uwezo wa kuzaa.

Siku chache zilizopita Mtangazaji wa Clouds Fm, Diva The Bawse aliweka wazi matatizo yake ya kutozaa na kuomba msaada kwa Watanzania toka hapo Sabby Angel naye ameibuka na kudai Yupo Tayari kusaidia mastaa.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers , Sabby aliyewahi kudaiwa kubanjuka kimapenzi na mastaa kadhaa akiwemo Alikiba alisema kuwa, anajua kuwa wapo mastaa wa kiume walio na wapenzi wao wenye matatizo kwenye kizazi kwa hiyo yupo tayari kuwabebea mimba.

Sitafuti kiki ila nimeeleza kitu ambacho nimekuwa nakifikiria muda mrefu baada ya kuona watu wengi wakiwemo mastaa hapa Tanzania kuwa na tatizo katika kizazi, mara mimba zinatoka na wengine kushindwa tu kubeba kwa sababu mbalimbali na ndiyo maana nikaamua kuongea hivi.

Zipo njia za kitalaamu unapandikiza mwisho wa siku unakuwa na mtoto wako ila kwangu kwa sharti moja tutasaini mkataba ambao sio chini ya milioni ishirini ili kupandikiza hizo mbegu kwa kuwa si unajua uzazi unachakaza sometimes kwa hiyo lazima nipate hela za kujitengeneza”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.