Sabby Angel Adaiwa Kutekwa na Penzi la Staa Nchini Kenya

Msanii wa Bongo movie aliyegeukia muziki wa Bongo fleva Sabrina Omary maarufu kama Sabby Angel anadaiwa kutekwa na Penzi la staa wamuziki nchini Kenya Khaligraph.

Kwa muda mrefu sasa Sabby Angel amedai amehamisha makazi yake nchini Kenya kwa ajili ya kufanya sanaa yake lakini inasemekana amehamia kule kwa ajili ya penzi la staa wa nchini humo Kaligraph Jones.

download latest music    

Gazeti la Ijumaa Wikienda wanaripoti kuwa Kwa mujibu wa chanzo chetu cha karibu kutoka Kenya ambacho kinafanya kazi kwa karibu na Khaligraph, wawili hao wapo kwenye uhusiano na ‘root’ nyingi za Kenya za Sabby anakwenda kwa mshikaji huyo.

Baada ya tetesi hizo kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii gazeti hilo lilimsaka Mrembo huyo na alifunguka haya:

Jamani watu mbona wambea hivyo! Kiukweli mimi nipo Kenya na kwa sasa muziki wangu ninafanyia huku lakini kuwa na uhusiano ha Khali, si kweli. Nina mtu wangu huku nninayefanya naye kazi lakini si yeye“.

Lakini Sabby alipotakiwa kumtaja huyo mpenzi wake alishindwa na kukata kata kata.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.