Saida Karoli afunguka kuhusu kazi yake na Diamond Platnumz

Muimbaji mkongwe Saida Karoli amefunguka kukiri kuwa ameweza kufanya vizuri na wimbo wake mpya, Urugambo.

download latest music    

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa katika album yake mpya amemshirikisha Bella 9 na Diamond Platnumz. Akizungumza kwenye interview Saida Karoli alisema kuwa hizi projects zake ambazo zitawatoa mashabiki jasho.

“Urugambo nimetoa kama zawadi kwa Watanzania, niliona nijitambulishe kama chai ya asubuhi, lakini watarajie mambo makubwa kwani hivi karibuni mimi na Belle 9 tutatoa kazi ambayo itawatoa jasho mashabiki wa muziki,”

Muimbaji aliendelea kudai kuwa kwa hivi sasa anapanga kuachia nyimbo nyingi kali ili kuwakumbusha mashabiki wake alivyokuwa hapo mbeleni. Pia anapanga nyimbo kufanya vizuri kwa sababu kwa hivi sasa Kuna wasanii wa Kisasa ambao anapaswa kuwafikia kimziki.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua