Sanaipei Tande awasihi wasanii wa Kenya kuandika nyimbo zenye ‘content’ za kuelimisha jamii

Image: Sanaipei Tande

Sanaipei Tande sasa hivi ameanza kurudi kwenye muziki baada ya kuchukua break ya muda mrefu. Ata hivyo bado sauti na nyimbo zake ni za kutoa nyoka pangoni.

Hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya ‘Amina’ ambao aliuachia wiki chache zilizopita. Sanaipei amekuwa akiupromote kupitia interview za radio na Televisheni. Ata hivyo aliweza kuzungumza na Bongo 5 ambapo alifunguka kusema kuwa wasanii wa Kenya wamepoteza muelekeo wa nyimbo zao.

download latest music    
Sanaipei Tande
Sanaipei Tande

Na kama wasanii ni jukumu letu kuleta mambo kama haya machoni mwa watu, ila kuimba tu bila maana inasaidiaje jamii!

Aliendelea kwa kusema kuwa wasanii wanapaswa kuachia muziki wenye maudhui. Sanaipei anahisi kuwa wasanii wakipoteza muelekeo kwenye nyimbo zao basi pia Jamii iankosa watu wa kuielekeza.

“Lazima pia tutengeneze miziki ya kuelimisha watu wetu na ‘Simama Imara’

Aliongeza kusema kuwa hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya May.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua