Sanchi- Ni Hobi Yangu Kuposti Picha Zangu Za Utupu

Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi kuwa anapendelea sana kuposti picha zake za utupu.

Sanchi alijipatia umaarufu kutokana na umbile lake na jinsi ambavyo amekuwa akipenda kupiga picha zake za kihasara hivyo kumfanya ajulikane sana ndani na nje ya Bongo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers Sanchi amefungukia suala lake la kupiga picha hizo za utupu na kudai hiyo ni moja kati ya hobi zake na anapenda sana:

Unajua kuna mtu mwingine anaweza kudhani nafanya makusudi lakini ndiyo hobi yangu. Hata nguo ambazo navaa huwa ndiyo roho yangu inapenda nivae hivyo na siyo za nusu utupu kama watu wanavyosema.

Na ukijaribu kunifuatilia utagundua kuwa nimebadilika sana kwenye suala la uvaaji kutokana na maneno ya watu”.

Lakini pia Sanchi amekana taarifa za yeye kuendesha maisha yake kutegemea kalio na kudai anategemea akili yake:

Mimi namshukuru Mungu kwa kunipa umbo hili ambalo ni la asili kabisa. Hao wanaosema nategemea kalio kuendesha maisha yangu ni ‘mabogasi’. Akili yangu ndiyo inayoniongoza katika maisha yangu, kama ni shepu mbona wengi tu wana shepu lakini hawana mafanikio kama yangu?”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.