Sanchoka: Makampuni Ya Kutengeneza Filamu za Ngono Yananiwinda Sana

Mrembo Jane Rimoy maarufu kama Sanchoka au Sanchiworld anayetikisa Bongo kwa sasa kutokana na umbo lake na picha zake za utupu anazopiga amefunguka na kueleza changamoto anazopata kutoka na umbo lake hilo na umaarufu alionao.

Kwenye mahojiano yake na Global Tv, Sanchoka amefunguka na kudai kuwa watu wengi wakimuona anapiga picha zake za mitego wanahisi kuwa labda anajiuza kitu ambacho si cha kweli bali anapiga vile kwa kazi zake za u-model anaofanya mara nyingi nchi kama Ghana, South Africa, Kenya na Nigeria, pia amedai watu makampuni mengine ya filamu za ngono yamefikia hatua ya kumtafuta ili akacheze filamu zao:

download latest music    

Unajua kama mwanamke kuna mambo mengi unaweza ukafanya tofauti na kujiuza na bado ukapata hela coz ni jinsi tu ya kucheza na akili za watu na ujue watu wanataka nini sio kwamba mtu akivaa nusu uchi akapiga picha basi anajiuza hiyo ni akili ya watu wengi wa Afrika yaani wanaona mtu kama mimi napiga picha vile nimevaa nguo za ndani tuna kuonyesha viungo vya mwili wangu basi wanajua nataka kujiuza lakini huko tunakoelekea naomba niamini tutaamini kwa sababu mwisho wa siku hao mnaosema wanajiuza ndo watakuja kufanikiwa na kufanya vitu vikubwa mshangae”.

Pia Sanchoka alielezea usumbufu anaopata kutoka kwenye makampuni ya kutengeneza filamu za ngono:

Makampuni mengi ya kutengeneza movie za ngono ya nje ya Tanzania hadi Marekani wengi tu wameshanitafuta wananiambia nitaje pesa ninayoitaka nifanye nao kazi lakini mimi sio mtu wa aina hiyo ndo maan nasikitishwa na uzushi wa watu wanaodai mimi najiuza kwa milioni moja ni kitu ambacho siwezi kabisa kwani hiyo ni pesa ndogo na isitoshe sijawahi hata kufikiria kujiuza kwa hela yoyote duniani kwani hayo sio malengo yangu wala wakati napiga hizo picha sijawahi kuwaza kutafuta wanaume”.

Sanchi aliweka wazi mwanaume anayeweza kutembea naye ni yule anayejishughulisha, anayejituma na siyo lazima awe na kipato kikubwa sana lakini awe anajitahidi awe ana malengo ya kufika mbali zaidi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.