Sarah,mpenzi wa Harmonize amjibu Wolper

Ikiwa ni  siku moja tu imepita tangu Harmonize na Wolper waingie tena kwenye bifu  zito baada ya msanii huyo wa lebel kubwa nchi ya wasafi kutoa wimbo ambao ulilenga kutoa siri za mahusiano yake na mpenzi wake huyo wa zamani Wolper ,wawili hao walijikuta katika malumbano mazito ambayo mpaka sasa yanaendelea mitandaoni huku kila mmoja akikataa kushindwa na kunyamaza ,katika post yake aliyotoa jana katika ukurasa wake wa instagram wolper aliandika kumshauri harmonize kuacha kuandika nyimbo ambazo zinamuhusisha yeye bali ajitaidi kuandika nyimbo ambazo hata zitakuwa zikimsifia mpenzi wake mpya anaejulikana kwa jina la sarah, pia Wolper aliandika maneno yaliyodhihirisha kuwa harmonize alimfata Sarah kwa sababu ya pesa.

Akitoa majibu ya post ya Wolper ,Sarah  aliandika hivi katika ukurasa wake wa instagram ” kama nilimpa hela nyingi akakuacha na wewe si umpe hela akurudie”, mwanamke huyo  wa Harmonize alikuwa kimyaa kipindi chote cha malumbano ya wawilio hao lakini sasa nae kaamua kufunguka ,hata hivyo Sarah pia alionesha dharau kwa kumwita mpenzi mpya  wa wolper “msukule”, “mbeba pochi” .Sarah ambae aliambiwa na Wolper kuwa hajui lugha leo anaamua kusema kuwa post hiyo ameiandika kiswahili kwa msaada wa mpenzi wake harmonize na kumtagi kabisa,” nimeandika kiswahili kwa msaada wa Harmonize”

download latest music    

Hata hivyo vita hiyo ya kimtandao sasa inaonekana kuwa kubwa kwa sababu imekuwa ni kati ya Harmonize na mpenzi wake Sarah huku Jackline Wolper ,  na inakuchukua taswira mpya kwasababu inakuwa kama kila upande  unaokuwa na wivu  na upande mwingine.

Ikumbukwe kwamba wawili hao wameachana muda mrefu lakini vita hii imeanza upya baada ya Jackline wolper kuamua kufunguka sababu ya kuachana na harmonize ambapo kati ya mengi aliyoyasema alisema kuwa mwanamke mpya  ambae ndio sarah alikuwa chanzo cha yeye kuachana na mwanaume huyo huko pia hela imetajwa kama kivutio cha mapenzi kutoka kwa mwanamke huyo.Je mpenzi mpya wa Wolper ataingilia kati, au watayamaliza wenyewe….

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.