Sasha Atishiwa Kuuliwa Baada Ya Kuiba Mume Wa Mtu

Video vixen maarufu kutokana na umbo lake Sasha Kassimu amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutishiwa maisha yake na mwanamama Aliyedaiwa kumpora mume.

Sasha amekimbilia kituo cha polisi cha Mtongani jijini Dar akidai kuwa, mwanamke mmoja aliyemtaja kwa jina la Mama Aisha anatishia kumuua.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers Sasha alikiri kuna muda aliwahi kudaiwa kuiba mume wa mwanamke huyo na tangia hapo amekuwa akipokea vitisho  mbali mbali juu ya maisha yake:

Huyu mama (mama Aisha) alipoachana na mumewe, akadai eti mimi ndiye nimemvunjia ndoa, nikashangaa sana lakini hivi karibuni nimepata taarifa kuwa anapanga kunimwagia tindikali.

Nilipata hofu sana lakini jamani labda leo niseme ukweli kwamba sikuwa na uhusiano na mume wa mama huyu, nilikuwa naenda pale nyumbani kwake maana dada yangu anaishi jirani.

Yeye anashikilia kuwa mimi nilionekana nyumbani kwake kwenye kochi, ni kweli kabisa ila ulitokea msiba, nikawa naogopa kukaa kwa dada yangu, ndo’ nikaenda pale nyumbani kwa yule baba kama jirani tu lakini hakuna ishu ya mapenzi, aache kuniwazia mabaya kabisa,

Nimeona nisikae tu maana linaweza kunitokea lolote, nimeenda kufungua jalada kwenye kituo cha Polisi cha Mtongani lenye namba MT\ RB\1477\2018 KUTISHIA KUUA KWA MANENO”.

Baada ya Tuhuma hizo gazeti hilo lilimsaka Mama Aisha ambaye alifunguka kuwa hajawahi kusema kuwa anataka kumwagia tindikali lakini amekiri kuwa Sasha amevunja ndoa yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.