Shamsa Ford afunguka kuhusu skendo ya ujauzito

Msanii wa Bongo Movies, mrembo na ambae anafanya vizuri katika tasnia hii ya filamu  kwa muda mrefu ,mwanadada Shamsa Ford amefunguka na kusema ukweli kuhusu tetesi zinazizidi kusambaa mitandaoni kuhusu yeye kuwa mjamzito , Shamsa ambae  amefunga ndoa hivi karibuni ikiwa ni kama  mwaka tu umepita  tangu ndoa yao na mumuwe   Chid Mapenzi  ameamua kusema ukweli  na kukanusha kuhusu tetesi hizo,Shamsa amekanusha kabisa taarifa izo na kusema kuwa hayo ni maneno ya watu tu katika mitandao wakitaka kumzushia kuhusu taarifa hizo.

“am not pregnant, mimi kweli kabisa sina  mimba” aliongea Shamsa  huku akicheka.

download latest music    

Kwa muda sasa kumekuwa na  tetesi mitandaoni huku watu wakisema kuwa Shamsa  ni mjamzito ,lakini Shamsa anakataa na kusema kuwa labda kwa sababu amekuwa akionekana mnene sana kwa muda sasa ndio maana watu wameanza kuhisi kuwa yeye ni mjazito,lakini unene wake ni kwasababu amejiachia na kula sana.

Hata hivyo Shamsa anaongezea kuwa inawezekana watu wanashawishika kuwa yeye ni mjamzito kutokana na picha zake alizopost hivi karibuni ambapo moja inamuonyesha amevimba uso kidogo na huku nyingine ikimuonesha akiwa  na mtoto wake wa kwanza wa kiume ikiwa na caption ya kusema anatamani kupata mtoto mwingine maana huyo aliyenae ameshakuwa.

Shamsa anaongezea kwa kusema kuwa watu wengi wamezoea kuwa mtu akishaolewa basi kinachofuata ni mimba na mtoto,lakini kwa upande wao bado hawajapanga kuzaa kwa sasa bado wanatafuta maisha mungu akujalia basi watapata mtoto “mimba ni jambo la kheri,kwanini nifiche,..nikipata basi Inshallah ”

Alipoendelea kuulizwa na mtangazaji wa kipindi cha eNews cha EATV ,kwamba kwanini watu wanasema wanamuona hadi anaenda kliniki Shamsa anasema hajawahi kwenda kliniki na ikitokea amepata mimba hawezi kufika  na kwasababu mimba inakuwa basi tumbo haliwezi kufichika.

Shamsa ameolewa ni mwaka mmoja  umepita tangu akiwa amefunga ndoa yake na kwa sasa anamtoto mmoja wa kiume anaeitwa Terry, na kama kweli Shamsa ni mjamzito basi tunamtakia afya njema yeye na mtoto wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.