Shamsa Ford Ahaidi Kujituliza Kwenye Ndoa

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka kuhusu mipango yake ya kujituliza kama mwanamke hasa kwenye ndoa yake.

Shamsa ameweka wazi kuwa mambo yasiyo sahihi amefanya sana, lakini kwa sasa umefika wakati wa yeye kutulizana hasa kwenye ndoa .

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyefanya na gazeti la Amani, Shamsa alisema kuwa, kutokana na kubadilika kitabia anatamani yeye na mume wake wawe mfano imara kabisa kwa jamii yaani waishi muda mrefu sana mpaka Mungu atakapowatenganisha.

Maisha siku hizi ni mafupi sana, ni muhimu mtu siku ukiondoka uache alama nzuri na ili hilo lifanikiwe ni muhimu kutulizana, jambo ambalo nimeamua kulifanya kwa sasa”.

Wasanii wengi wamekuwa wakiongelea kutulia na kuomba dua  hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.