Shamsa Ford Ahofia Kuachika ‘Mapenzini’ Kama Zari

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Shamsa Ford amefunguka kuhusiana na mambo ya mapenzi na kuweka wazi uoga wake inapokuja suala la kuachwa.

Shamsa Ford Amekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri kwa wanawake wengine kuhusu masuala ya kudumu katika ndoa na ni juzi tu aliwaasa mastaa wenzake kujitahidi na kutoingiza ustaa Kwenye Mahusiano n ndoa zao.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe ambao ambao ameonyesha hofu yake kubwa endapo atakuja kuachana na mume wake mfanyabiashara maarufu Chiddi Mapenzi aliyefunga naye ndoa mwaka juzi.

Shamsa ameonyesha uoga wake lakini ameweka wazi anaogopa ua jeusi ambalo liliwekwa na Zari alipomtosa Diamond ili kuashiria penzi lililokauka au kuishiwa.

Mwenyezi Mungu niepushie na hili UA na huu uzee nitaenda wapi.. inatisha khaaaa”.

 

Zari aliweka rekodi na kulipa umaarufu UA hilo jeusi baada ya kulitumia kuvunja Mahusiano Yake na Diamond siku ya Valentine’s Day mapema mwaka huu.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.