Shamsa Ford Ajibu Tuhuma Za Kumfilisi Chidi Mapenzi

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amejibu tuhuma ambazo amekuwa akitupiwa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amemfilisi mume wake Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mfanyabiashara maarufu sana wa nguo na viatu Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuwavalisha mastaa kibao ikiwemo Diamond na wengineo.

download latest music    

Lakini tangu Chidi afunge ndoa na Shamsa ameonekana kufulia kupita kiasi na haishi maisha aliyokuwa anaishi mwanzoni ambapo alikuwa anaonekana na duka kubwa na magari mazuri jambo lilipelekea watu wengi kumtuhumu Shamsa kamfilisi Chidi tangu amuoe.

Kwenye Interview na Enews ya EATV Shamsa amekana tetesi hizo na kuweka wazi kuwa maisha aliyokuwa anaishi Chidi siku za nyuma yalikuwa ni ya anasa na ujana mtupu hivyo walivyofunga ndoa alimsihi abadilike ili waweze kuweka akiba na hata kumsaidia kupunguza marafiki wasiokuwa na maana.

Lakini kuhusu duka kufilisika, Shamsa ameweka wazi kuwa walikuwa duka kubwa na la kifahari lakini walikuwa hawaingizi faida kubwa kwa sababu kodi ilikuwa kubwa hivyo akamshawishi mume wake wahamie Kwenye duka Dogo ili waweze kumudu kodi.

Lakini pia Shamsa ameweka wazi kuwa yeye sio mtu wa kupenda Show off kwa watu aonekane anaishi maisha ya kifahari ili Apate umaarufu Hapana anaishi kwa uahalisia wake kwa kile alichokuwa nacho kiukweli kabisa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.