Shamsa Ford atoa onyo kali kwa vijana wanaofugwa na kinamama wanaowazidi umri

Muigizaji wa filamu za Bongo Shamsa Ford amewasuta vijana ambao wanaingia kwenye mahusiano na kinamama wanaowazidi umri.

Staa huyo ameonyeshwa kukerwa na tabia hio kwani anasema vijana wanakua wazembe na kuishi kutegemea kulishwa na kufanyiwa kila kitu bila ya wao kutoa jasho.

download latest music    

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki. Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah,” Shamsa Ford aliandika kwa mtandao wa Instagram.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere