Shamsa Ford Awataka Mastaa Wenzake Waache Kuchukuliana Wanaume

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewajia juu mastaa wenzake kwa vitendo chao vya kuchukuliana mabwana/ Waume bila kujali jinsi vitendo hivyo vitakavyoumiza wengine.

Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa yeye binafsi hakuna kitu anachokiheshimu kama ndoa ya mtu au Mahusiano ya mtu mwingine kwaiyo hawezi kuingilia hivyo lakini anashangaa watu wanaokosa utu na Kuiba mabwana wa watu.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Amani bila kuwataja majina, Shamsa alisema kuna baadhi ya mastaa wanajua wazi mwanaume anayemtongoza ni wa rafiki yake lakini akijua tu ana fedha yuko radhi hata ajifanye kama hamjui huyo rafiki yake ili mradi tu atembee naye.

Mimi jamani niko tofauti kabisa siwezi mwanaume wa rafiki yangu akanitongoza nikakubali ninaheshimu hilo lakini wengine wako radhi wakukane ili mradi tu apate fedha”.

Lakini pia Shamsa ameweka wazi kuwa yeye hana wasi wasi wa kuibiwa mume wake Chiddi Mapenzi kwani anamuamini mume wake kuwa ni mwaminifu.

Lakini pia siku za nyuma Shamsa alikwisha weka wazi kuwa hawezi kumuacha mume wake kwa sababu ya michepuko baada ya kujulikana alikuwa anachepuka.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.