Shamsa Ford Awatupia Madongo ‘Wanaume wa Dar’

Image: Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Shamsa Ford ameibuka na kuwatupia madongo wanaume wa Dar.

Shamsa amewasema vijana ambao wamekalia kuwa vibenten ambao wanategemewa kulelewa na wanawake wenye pesa kutoka na kukosa elimu ya kuweza kuwakwamua.

download latest music    

Shamsa alitokwa na povu hilo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alidai mbali na kuwa vibenten bali wengi wao ni wambea na chawa:

Wanawake wenzangu tujitahidi sana kuwapa elimu ya kutosha watoto wetu wote haswa watoto wa kiume. Nimejikuta kuwa na huruma zaidi na watoto wa kiume kwasababu wa kwangu ni wa kiume. Huwa naumia sana nikiona mtoto wa kiume anavyoangaika kupata riziki”.

Lakini pia shamsa ameendelea kusema kuwa wazazi lazima wahakikishe wanawapa elimu watoto wao na yeye kama mzazi atahakikisha anatimiza hilo:

Mtoto wa kiume asipokuwa na elimu ya kutosha au ujuzi wowote mwisho wao huwa ni mbaya kuliko watoto wa kike. Sasa hivi vijana wengi ambao hawana kazi au hawakubahatika kusoma ndo WAMBEA,WAPAMBE,VIBENTEN MARA CHAWAAA.

Kuwa mwanaume ni heshima kubwa sana kama ukisimama kwenye misingi ya kiume..Nitauza vitumbua, madira hata kufagia barabara ilimradi mwanangu apate elimu”.

Shamsa ni mama wa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Terry.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.