Shamsa Ford:Naheshimu Sana Ndoa Yangu

Msanii wa filmu tanzania Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa hata siku moja hawezi kufanya upumbavu wa kuharibu ndoa yake kwa mabo ya kijinga au kumkazwa mume wake .Shamsa amesema kuwa kama na yeye angekuwa anataka kujivika ustaa na kuacha kuheshimu ndoa yake mpaka sasa angekuwa ameshaachika kama wasanii wengi wa kike wanavyoachika na kushindwa ndoa.

Shamsa anasema kuwa alipoamua kuolewa aliamua kujishusha kabisa na kufanya yale yanayotakiwa katika ndoa kwa sababu aliamini kabisa kama angeendekeza ustaa basi ndoa ingekuwa ilishamshinda siku nyingi.Shamsa anasema kuwa katika ndoa kuna vitu lazima mwanamke uvilinde na ndio maana hata yeye ameweza kudumu na kuachana na mambo ya usanii.

download latest music    

Siwezi kufanya ujinga wa kuichezea ndoa yangu hata siku moja,kwani ndoa ni kitu adimu sana kwaio unapokipata lazima ukilinde na kukitunza vizuri sana.kama ni ustaa nauacha mlangoni, ninpoingia nyumbani kwangu nayaacha yote la sivyo ndoa yangu isingedumu hata siku moja.

Shamsa aliolewa mwaka juzi na moja ya watu wanaopendezesha wasanii jijini Chidi Mapenzi na amedumu katika ndoa hiyo tangu amefunga ndoa.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.