Shetta Afunguka Sababu ya Ruby Kutolewa Katika Uongozi Wao

Kuna habari nyingi sana zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mwanadada Ruby amefukuzwa katika uongozi wake mpya kwa sababu ya utovu wa nidhamu na wasanii wengi waliongelea swala hilo huku wakimtaka mwanadada huyo kutulia na kufanya kazi na watu.

katika baadhi ya sababu za kufukuzwa kwa Ruby katika uongozi wake mpya ilisemekana kuwa shetta alikuwa sababu. na kwa mujibu wa Ruby kwa maneno yake ya chini chini alikuwa akimlalamikia msanii mwenzake huy.

download latest music    

Sasa basi akiongea na Clouds Media , Shetta anaelezea hali ilivyokuwa mpaka kufanya ruby kufukuzwa katika uongoiz wao mpya , anasema “siwezi kusema kuwa mimi ndio sababu lakini sisi ni wanafamilia na tunakwaruzana maana hata wachawi pia wanagombana wanapokuwa wanawanga, kulitokea mpishan wa kauli kati yak na meneja, na nilimwambia kuwa yule ni kiongozi anahitaji heshima, lakini ruby alinvamia mimi, kwaio nikamwambia chambuso amuandikie barua ya kumsimamsiha kwa muda kwa utovu wa nidhamu.”

Hata hivyo Shetta anasema kuwa barua hiyo iliuwa ya muda na walitegema kuwa muda ukifika basi atarudi kwa ajili ya mazungumzo alkini wameshagaa ameamua kufanya kazi zake mwenyewe.

Ruby aliwahi kutajwa sana kuwa ni msanii anaekosana na viongozi wake mara nyingi kutokana na swala hilo la nidhamu, wasanii wengi wakubwa wamewahi kuongelea swala lake wakitaka ajirekebishe.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.