Shilole atangaza harusi baada ya kutolewa posa

Image: Shilole

Kuna fununu kuwa msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au ‘Shishi Baby’ ametolewa posa na mchumba wake ambaye bado hajamjulisha kwa mashabiki wake.

Kulingana na chanzo kilicho ongea na Ijumaa Wikienda inasemekana kuwa shishi hataki watu wakimjua mwanaume wake kwa ajili anataka kuiweka ndoa yake iwe Siri, chanzo hicho kilisema;

download latest music    

“Si unawajua tena mastaa wetu? Hawachelewi kufanya yao ndiyo maana Shishi hataki kumwanika mwanaume wake kwa madai kwamba anaogopa wajanja wasije wakapita naye kama ilivyo kwa yule aliyekwapuliwa na Nisha (mwigizaji Salma Jabu).”

Aliendelea kwa kusema;

“Baada ya mbilingembilinge nyingi za mjini, hatimaye Shishi sasa anaolewa na hapa tunapoongea ndiyo kwanza watu wamerudi Dar kutoka Igunga (Tabora) nyumbani kwa akina Shishi kupeleka posa. Kwanza ishu ilikuwa ni kumtambulisha mwanaume kwao ndipo wakaona wamalize kabisa na suala la posa hivyo kifuatacho ni kufunga ndoa ambayo nasikia itakuwa ndani ya mwaka huu,”

Hata hivyo Ijumaa Wikienda ilipompigia Shishi kujua kama ni ukweli alifunguka kusema;

“Wewe ujue tu ni kweli nimechumbiwa lakini kuhusu kumwanika mtarajiwa wangu, kwa kweli sipo tayari. Maana kwa upande wa wanaume wanaonyatia wanawake wa watu wanaitwa Team Fisi, sasa sijui kwa upande wa wanawake. Au tuseme Team Fisi kwa upande wa wanawake.”

Aliendelea,

“Lakini kimsingi mchumba wangu ni mtu wa kawaida sana na siyo staa,” alisema Shishi na kutoa mwanya kwa mahojiano zaidi kuhusu ishu hiyo.

Kuhusu harusi yake Shishi alisema,

“Mashabiki wangu wajue tu itakuwa soon na itakuwa ya aina yake kwani itafanyika uwanjani na mashabiki wataingia kwa kadi. Mchango utakuwa mdogo ili watu wengi zaidi wahudhurie.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua