Shilole Kuachana Na Vi-ben Ten

Mwanadada mrembo kabisa, jasiri na mpambanaji, anefanya vizuri katika muziki wake, Zuwena Mohamed  almaarufu kama Shilole, amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hivi mapenzi na vi-ben ten anasimama kwanza kwa sababu havimpi faida yoyote.Shilole amefunguka na kusema kuwa alichogundua na kwamba hakijikita katika mapenzi hayamzalishii chochote lakini akijikita katika kazi anaona matunda yake hivyo kwa sasa bora afanye kwanza kazi.

“Jamani kwa usawa huu mtu hasipobadilika  na kuangalia kitu cha maana ni shida sana, mimi binafsi  mambo ya mapenzi sijui na vi ben ten vikae kwanza  vinisubirie kwanza huko, nifanye kazi zangu ili nipate kwanza maendelea yangu, sio mapenzi wanafaidi watu wa instagram tu,kukuangalia kila siku maisha yako.” alisema Shilole

download latest music    

Shiloleh ni moja wa wasanii wanaoingia kwenye kundi la wanawake wanaojiingiza kwenye mapenzi na vijana wanao wazidi umri,kwa  kipindi kirefu mwanamuziki huyo amekuwa akikumbwa na scandal za kutembea na vijana wanaowazidi umri na kuwatesa kwa sababu tu anawapa ela, mfano alishawahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzie Nuh Mziwanda na baadae walikuja kuachana ambapo Nuh aliongea mambo mengi ya mahusiano yao ikiwa na lile la kuwa kipindi cha mahusiano yao alikuwa  hana sauti kwa mwanamke huyo.

Shiloleh  ambae kwa sasa yupo na uhusiano wa kimapenzi na kijana  Uchebe   inasemekana kuwa alikuwa  mume wa mtu lakini alikuja kumuacha mkewe kwa talaka kwa sababau ya kuishi na  Shiloleh pia ni kijana mwenye umri mdogo kuliko mwanadada huyo.Wawili hao wamekuwa wakionekana kuwa pamoja kwa muda mrefu na kusema kuwa hawategemei kuachana.

Ukiachana na kazi ya muziki, Shilole aliona fursa ya biashara ya chakula kwa upande mwingine na kuamua kuisogelea, biashara ambayo inamfanuy akukutana na mashabiki wengi zaidi na kuwa karibu na wateja wake pia.Pamoja na maneno mengi yanayozunguka mitandao juu yake Shiloleh ni mwanamke jasiri na anaeyeonekana kupitia mengi kwenye maisha kabla ya hapo hivyo kwa sasa yeye amuamua kufanya kazi tu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.