Shiloleh Na Uchebe Kufunga Ndoa,Honeymoon Ulaya

Mume mtarajiwa wa msanii Shiloleh, mwanadada ambae amekuwa ni moja ya wanawake wapambanaji katika maisha  amefunguka na kuongelea mipango yao ya harusi inavyokwenda na jinsi harusi iyo itakavyo fanyika.Mwanaume huyo anaejulikana kwa jina moja la Uchebe amesema kuwa mpiango ya  harusi ipo karibuni lakini nia yake kubwa katika harusi hiyo ni kumpeleka mke wake huyo Ulaya kwa ajili ya honeymoon yao.

Akiongea na East Africa, Uchebe amesema kuwa ndoa yao hiyo inategemewa kufungwa mwezi wa kumi na mbili(12) mwaka huu  kwa sababu yeye na mkewe mtarajiwa wameshakubaliana kabisa na taratibu za ndoa zimeshaanza kufanyika  na wanataka kuhararisha mahusiano yao.

download latest music    

“Mwenyezi Mungu ameshafanya wepesi  sasa hivi tupo katika  kwenye maandalizi, na Mungu akipenda mwezi wa kumi na mbili itakuwa ndoa kamili kwani taratibu zote nishazifuata,mahari nishatoa sidaiwi kabisa na honey moon nampeleka Ulaya” amesema Uchebe ambae ndie mume mtarajiwa wa Shiloleh

Uchebe ambae sasa hivi ni mume mtarajiwa wa Shiloleh, alishawahi kuwa na ndoa kabla ya hii inayoenda kufungwa sasa, ambapo inasemekana kuwa ndoa hiyo ilivunjika baada ya mwanaume huyo kuingia katika  mahusiano  na Shiloleh.

Ingwa kwa hivi karibuni pia kulikuwa na tetesi za wawili hao kuwa wameachana baada ya Shiloleh kusema kuwa yeye na vi-ben ten sasa basi, taarifa za kuachana kwao wamezikanusha na kusema bado wanaendelea  na mahusiano yao na kwa sasa wapo katika mipango ya harusi.

Mwanadada Shilole ni moja ya wasanii wa kike wenye kupendwa na mashabiki wengi sana lakini pia ni moja ya wasanii wenye ushawishi  mkubwa sana  kwa mashabiki wake.Ukiachana na kazi ya muziki anayofanya Shiloleh pia ni mama ntilie anaepika chakula mwenyewe na kuwahudumia wateja wake mwenyewe.Amekuwa ni mwanadada anaeangaliwa sana na watu na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wengine.

Ingawa kumekuwa na maneno yanayomkabili kuhusu tabia yake ya kutemba na vijana wenye umri wa chini yake , lakini hajawahi kuathirika na maneno hayo zaidi ya yeye kupiga kazi ili kuwaridhisha masbabiki wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.