Shiloleh Afunguka Anachopenda Kwa Uchebe

Msanii wa musiki wa bongo fleva shiloleh amefunguka na kutaja mambo anayoyapenda kwa uchebe na jinsi gani amekuwa moja ya wanaume wanaomsapoti na kumjali sana kimaisha pamoja n kwamba watu wamekuwa wakisema kuwa hawatadumu kutokana na ukweli kwamba mara nyingi  amekuwa hadumu na wanaume katika mahusiano.

Shiloleh anasema kuwa anashukuru mungu kwa sababu pamoja na skendo nyingi alizowahi kuzipitia kabla ya kumpata uchebe lakini ameweza kukubalika ukweni (kwa wazazi wa uchebe).

download latest music    

ninashukuru mungu sana wakwe zangu ni wacha mungu na wananielewa sana na mimi ninawaelewa sana,hawapendi kusikiliza maneno ya watu wanatambua muda wa kazi ni upi na  na muda wa nyumbani ni upi hivyo tunaishi kizungu.

Hata hivyo shiloleh anaendelea kwa kusema kuwa kipindi cha nyuma alikuwa hajatulia kwa sababu alikuwa anatafuta mwanaume wa kutulia nae ila kwa sasa anatulia kwa sababu anaamini kwa uchebe ndio amefika.

unajua kipindi cha nyuma watu niliokuwa nao wote walikuwa wanataka niendelee kujichetua,sikuwa na mtu sahihi wa kuniongoza lakini nilipompata uchebe tu alianza kuwa ananikosoa, na kunirudisha katika msati ulionyooka, na ndio maana sasa hivi nimebadilika sipo kama zamani.

nilikuwa nahitaji mtu ambae atakuwa ananikosoa pale ninapokosea kila mara,lakini pia mtu ambae atakuwa ananijali mud wote na hivyo vitu nilikuwa nakosa mara ya kwanza.

Shiloleh aliendelea kumsifia mwanaume wake kwa kusemakuwa watu wanaweza wasielewe kila kitu anachoongea lakini anapenda sana kumuona Uchebe akicheka.

macho ya uchebe mie hoi,napenda sana tabasamu lake hasa pale anapocheka meno yake yote huwa hayaonekani.kwa mtu wa kawaida hawezi kuelewa lakini napenda  macho yake akitabasamu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.