Shiloleh:Sitakubali Mume Wangu Aoe Mke wa Pili.

Msanii wa muziki nchi na mjasirimali maarufu bongo kwa upande wa  wanamuziki ambae amekuwa akijituma sana katika kufanya kazi na kujilindia heshima yake mjini , Shiloleh amefunguka na kusema kuwa kamwe katika maisha yake haitakuja kutokea kumruhusu mwanamume wake kuoa mke wa pili eti kwa sababu anataka kusaidiwa majukumu.

Shiloleh anasema kuwa hakuna kitu kigumu kama ndoa ila watu tu hawajui, na kama mwanaume anashindwa kuyatuliza maswala yake katika ndo ya mke mmoja hawezi kutuliza kwa ndoa ya pili.Shiloleh anasema kuwa kamwe mume wake hatooa mke wa pili na hata yeye hawezi kukubali hata kama dini yao inaruhusu kwa sababu hata hiyo dini kuna mambo inataka mwanaume atimize akioa mke wa pili.

download latest music    

mimi mume wangu hawezi kuoa mke wa pili hata kama dini inaruhusu , na anaoa mke wa pili for how,mimi nina mapungufu gani kwanza mpaka aoe mke wa pili.mtu mwingine anaweza kuwa na mapungufu yake na huwezi kuyajua.kwaio mimi sina mapungufu yoyote.me wangu kamwe hawezi kuoa mke wa pili  hata kama dini inaruhusu hata hiyo dini inavyoruhusu kuna mambo anatakikana kuyajua na kuyafanya.

Mwingine anakwambia eti kuoa mke wa pili mbona kawaida tu,je unaweza kuyafanya yanayotakiwa ndani ya ndoa au, sio unaiona ndoa tu jamani ndoa ngumu.hawezi kuoa mke wa pili hata kama dini inaruhusu na kamwe sitakaa nikubali aoe mke wa pili.

Maneno ya Shiloleh ayankuja baada ya mwandishi wa Ayo Tv kumuuliza maoni yake kuhusu kile kilichosambaa katika mitandao wiki iliyopita  baaada ya mkuu wa Wilaya ya Pangani kuweka wazi kuwa yeye ndie aliyemruhusu mume wake kuoa mke wa pili ili aweze kumsaidia majukumu amo mume wake anakosa pindi anapokuwa katika majukumu ya kikazi serikalini.

Shiloleh na Uchebe wanatimiza zaidi ya miezi mitatu sasa tangu kufungwa kwa ndoa yao mwaka uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu na kupewa zawdi mbalimbali katika harusi yao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.