Sholo Mwamba- Man Fongo Ameshuka Kimuziki

Msanii mkali wa muziki wa Kisingeli Sholo Mwamba amemtolea povu msanii mwenzake Man Fongo ambaye amewahi kutamba na kibao chake cha ‘Hainaga ushemeji’ na kudai muziki wake umekufa.

Sholo Mwamba na Man Fongo ni wasanii ambao wana bifu la siku nyingi na bifu lao lilipamba moto baada ya Man Fongo kudaiwa kuchukua mpenzi wa Sholo Mwamba.

download latest music    

Lakini sasa Sholo Mwamba anamtolea povu mwenzake Kwenye Interview aliyofanya na Wasafi Tv ambapo amedai amefulia na muziki ambao alikuwa anaimba umeshakufa:

Sijui Man Fongo atakuja kunfanyia nini ili nije kuelewana naye kwani sahivi kama unavyoona sihitahi kukaa naye waka kuongea ongea naye na kama unavyoona kiupande wake wa muziki ameshuka kabisa tofauti na wasanii wengine wanaofanya muziki.

Anafanya muziki kama amechoka kichwa yaani anakopi nyimbo za zamani sijui Lau nafasi”.

Bifu kati ya wasanii hawa wa Kisingeli limekuwa likikiki kwa muda mrefu huku chanzo kamili kabisa hakijajulikana ni nini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.